Jumanne, 4 Machi 2014

PROFESOR IKONGO


HII NDIYO BARUA ALIYOANDIKIWA  ASKOFU BATENZI AMBAYE NI MWENYEKITI WA PCT AMBAYO KWA SASA BAADA YA KUGUNDUA WAMEJULIKANA NA SEREKALI WAMEBADILISHA JINA NA KUJIITA CPCT. KARIBU USOME BARUA INAYOFUATA HAPO CHINI.




 PENTECOSTE  PASTORS  FELLOWSHIP  TANZANIA

                                      ASKOFU  PIUS  ERASTO IKONGO
                                                            S.L.P  2730 DAR  ES                                                                  0788171176/0752558069
                                                       Email:pierako@yahoo.com
PENTECOSTOL COUNCIL
OF TANZANIA. PCT
P.O.BOX 62535
DAR  ES  SALAAM

YAH: KIKAO CHA PCT CHA TAREHE 26 NA 27 KUDAI ASKOFU IKONGO NDIYE ANAYE ICHONGANISHA SEREKALI NA PCT.

Baba  Askofu Batenzi Salaam.  kama kichwa cha Somo hapo juu ni Muhimu sana. Rejea kikao mlicho kaa na kunijadili nakuona ya kwamba mimi ndiye hasa ninaye husika kuichonganisha PCT na Serekali, na kupitisha eti kuuona uongozi wangu wa EAGT ili wawape ruhusa ya kuonana na mimi ili kunihoji juu ya swala hilo.

Mtumishi wa Mungu Baba Askofu nasikitika kusema kwamba Uongozi wa PCT umeshindwa kutambua ni nani mchonganishi wa PCT na Serekali kama sio hila na unafiki mnaweza kuchagua wenyewe.

Kwanza si kweli kwamba kuonana na mimi ili kuniuliza lolote ni lazima mpitie kwa Viongozi wangu wa EAGT kwani vikao vyote vilivyopita hamkufanya hivyo, bali mlinipigia simu au kuniita kwa njia ya SMS nami natii na kuja. Kupitia barua hii napenda kuwafahamisha Maaskofu na Wachungaji pamoja na Viongozi wote wa PCT ya kwamba Hizo ni mbinu za Uongozi wa Kitaifa wa PCT kuficha ukweli kwamba hawataki kuutambua Uongozi wa PPFT na kutambua kwamba mimi ndiye mwenyekiti halali  wa PENTECOSTE PASTORS FELLOWSHIP TANZANIA, NA KWAMBA KUMEKUWA NA MGOGORO MKUBWA KATI YA PCT NA PPFT. 

Mgogoro huu unatokana na Katibu Mkuu wa PCT kutumwa kwa Msajili wa Vyama vya Kijamii kuzuia PPFT Isisajiliwe, na hili sio kwetu tu, bali ninao ushahidi wa kutosha kwambwa Uongozi wa PCT umekuwa na tabia ya kujipendekeza kwa maslahi yao kwenda katika Ofisi ya Msajili kuishauri Serekali Isisajili Makanisa ya Kipentecoste bila kupitia kwao.

Na Watumishi wa Mungu wengi wameshindwa kupitia PCT kwa vile Ada inayolipishwa na PCT nikubwa kuliko ya Serekali. Serekali ni Tsh 20,000. kwa mwaka PCT ili kuwa mwanachama lazima ulipe 200,000. kwa mwaka.

Baba askofu Batenzi mimi EAGT ni Mshirika na Mchungaji tu, wa Kawaida ila mimi ni Mwenyekiti wa PPFT Kitaifa, Rejea kikao cha PCT NA PPFT Tarehe 28/3/2013 Ubungo Plaza na kukubaliana kwamba PPFT kwa vile Sio baraza bali ni Ushirika wa Wachungaji wa Kipentecoste hivyo PPFT itakuwa mwanachama wa PCT kwa sababu PCT ni baraza.

Natumia nafasi hii kuwaomba Maaskofu na Wachungaji wote wa Kipentecoste kutokubaliana na Ubinafsi, Unafiki wa Viongozi hawa wa PCT Wanaokaa vikao na kuomba kutafuta kuonana na mimi wakati tarehe 9 na tarehe 10 Waliniita kama kiongozi wa PPFT na kuhudhuria vikao hivyo.

Kikao cha tarehe 9 na 10 /2/2014 Niliwahoji sana kuhusu kama kweli wamepeleka Majina Ikulu watuonyeshe wajumbe wa kikao tujue ni majina mangapi na ni akinanani Wamependekezwa na PCT Kabla ya tarehe 11/2/2014 kujitokeza mbele ya Vyombo vya Habari ili Kuilaumu Serekali jambo ambalo mpaka tunaenda kukutana na Vyombo hivyo vya habari hawakutaka kuturidhisha Wajumbe wa kikao kwamba Majina yalipelekwa.

Na  hii ndio sababu mpaka leo Uongozi wa PCT haujaweka wazi kama walipeleka Majina Ikulu ni mangapi na ni akinanani.

KUHUSU MADAI YA ASKOFU  IKONGO KUICHONGANISHA SEREKALI NA PCT  SI KWELI.
Baba Askofu Batenzi nakuheshimu sana, ila kwa hili ni vema wewe ukiwa Mwenyekiti wa PCT Ukasema ukweli hata kama ukweli huo  utakugharimu ni vema kuusimamia na ndio sifa za Kiongozi Mcha Mungu na mwenye Hofu ya Mungu ambavyo ndivyo nilivyo kuwa na kuelewa.

Nakuomba unijibu Maswali yangu haya ndipo tutatambua Mchonganishi ni nani.

1.    Mwaka 2010 wakati wa Uchaguzi mkuu wa Serekali ni  nani alieandika barua kwa jina la PCT na kuisambaza Nchi nzima kuwa Serekali ya CCM isichaguliwe? Ni mimi au ni PCT ?

 
2.    Barua ya tarehe 19/3/2014 yenye maneno yanayosomeka nanukuu” HAKUNA SABABU YA SEREKALI ILIYOKO MADARAKANI KUENDELEA KUNG'ANG'ANIA KUONGOZA NCHI”  Barua hiyo Ilifikishwa Ikulu   Kwa niaba ya Wapentecoste wote Tanzania imesainiwa na Mwenyekiti wa PCT Taifa. Swali bado ni mimi naichonganisha PCT na Serekali?


3.    Barua ambayo ni Taarifa ya PCT  Taifa kwa niaba ya Wapentecoste wote Tanzania ya tarehe 11/2/2014 Inasema nanukuu “PCT ITATAFAKARI HATUA MADHUBUTI ZA KUCHUKUA DHIDI YA SEREKALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI” Barua hiyo imesainiwa na Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa PCT Taifa. Je bado mnadai Askofu Ikongo ndiye anaichonganisha PCT na Serekali?

Mwenyekiti nadhani huo ni ushahidi wa kutosha kwamba Uongozi wa PCT Taifa unafanya kila mbinu kuchonganisha Wapentecoste na Serikali kwani mimi siamini kwamba Matamko hayo hapo juu ni ya Wapentecoste wote Tanzania. Ni wazi kwamba Uongozi wa PCT Unajaribu kuhodhi Upentecoste kanakwamba nyie ndio mna hati miliki ya Upentecoste. Mtakuwa mnajidanganya wenyewe, kwani hata mambo ya msingi ya kuanzishwa PCT mmeyaacha na kuanza mambo yenu wenyewe bila hata kushirikisha Maaskofu wote na Wapentecoste Tanzania.
Nasikitika kusema hata Wokovu wenu ninamashaka nao, kwa vile Vongozi wa PCT Mmekuwa Waongo,Wabinafsi, na Wanafiki na kwa sababu mimi nawambia ukweli ndio sababu mnanichukia na kuanza kukaa vikao kunijadili. Kumbukeni mliwaambia Wananchi wote Tanzania kwamba Bonke anakuja Tanzania, nilipowaambia wambieni watu ukweli kwamba Bonke haji, mkazusha oo Ikongo mbaya, Mlichangisha Pesa za Waumini kwamba Bonke anakuja na ilipofika siku ya Mkutano Bonke hakuja Hamkutubu dhambi hiyo bali mlijifunika funika ili muendelee kula pesa za Wapentecoste. Leo hii Uongozi wa PCT hamko tayari kuweka wazi mapato na matumizi ya Pesa kiasi cha laki mbili kila mwaka kwa makanisa 75 wanachama wa PCT bali mnamtafuta mchawi wakati mnajiloga wenyewe.

Mwisho nimeamua kuandika barua hii na kuweka wazi kila kitu japo mengi nimeyaacha, baada ya Wewe Mwenyekiti kunieleza kwa njia ya simu kwamba lazima mtaniita na kunihoji katika kikao cha tarehe 26 na 27/2/2014 kinyume chake haukuniita na kuamua kunijadili katika kikao hicho kwa malengo ya kuficha ukweli na kunipaka matope kwa jamii ya Wapentecoste.

Kupitia barua hii nachukua nafasi kuwaomba Maaskofu na Wachungaji wote Tanzania walio wanachama wa PCT kuwa makini na Uongozi wa PCT kwani Wanaichonganisha Serekali na Wapentecoste Tanzania kupitia Matamko wanayoyatoa bila kuwashirikisha Wanachama.

Pia ningeshauri Kila Kanisa la Kipentecoste lililosajiliwa kihalali kuandika barua Serekalini ya kukanusha kwamba halihusiki na Matamko makali yaliyotolewa na Viongozi wa PCT , Na  yakwamba KANISA HUSIKA HALIKUBALIANI NA MALUMBANO NA SEREKALI. Ukihitaji barua za nakala za barua za matamko hayo makali na ya uchonganishi kati ya Makanisa ya Kipentecoste na Serekali nitakupatia.

Sina mengi Ila nawatakia Viongozi wa PCT Kutubu na kurejea kwa BWANA YESU.

Nakala
     Maaskofu wa Kipentecoste wote Tanzania
     Wachungaji wa Kipentecoste wote Tanzania
     Msajili wa Vyama vya Kijamii Tanzania
     Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais

PROF. PIUS ERASTO IKONGO
                                                        MWENYEKITI  PPFT TAIFA