HII NDIYO BARUA ALIYOANDIKIWA ASKOFU BATENZI AMBAYE NI MWENYEKITI WA PCT AMBAYO KWA SASA BAADA YA KUGUNDUA WAMEJULIKANA NA SEREKALI WAMEBADILISHA JINA NA KUJIITA CPCT. KARIBU USOME BARUA INAYOFUATA HAPO CHINI.
PENTECOSTE PASTORS FELLOWSHIP TANZANIA
ASKOFU PIUS ERASTO IKONGO
S.L.P
2730 DAR ES 0788171176/0752558069
Email:pierako@yahoo.com
PENTECOSTOL COUNCIL
OF TANZANIA. PCT
P.O.BOX
62535
DAR
ES SALAAM
YAH: KIKAO CHA PCT CHA
TAREHE 26 NA 27 KUDAI ASKOFU IKONGO NDIYE ANAYE ICHONGANISHA SEREKALI NA PCT.
Baba
Askofu Batenzi Salaam. kama
kichwa cha Somo hapo juu ni Muhimu sana.
Rejea kikao mlicho kaa na kunijadili nakuona ya kwamba mimi ndiye hasa ninaye
husika kuichonganisha PCT na Serekali, na kupitisha eti kuuona uongozi wangu wa
EAGT ili wawape ruhusa ya kuonana na mimi ili kunihoji juu ya swala hilo.
Mtumishi wa Mungu
Baba Askofu nasikitika kusema kwamba Uongozi wa PCT umeshindwa kutambua ni nani
mchonganishi wa PCT na Serekali kama sio hila na unafiki mnaweza kuchagua
wenyewe.
Kwanza si kweli
kwamba kuonana na mimi ili kuniuliza lolote ni lazima mpitie kwa Viongozi wangu
wa EAGT kwani vikao vyote vilivyopita hamkufanya hivyo, bali mlinipigia simu au
kuniita kwa njia ya SMS nami natii na kuja. Kupitia barua hii napenda
kuwafahamisha Maaskofu na Wachungaji pamoja na Viongozi wote wa PCT ya kwamba
Hizo ni mbinu za Uongozi wa Kitaifa wa PCT kuficha ukweli kwamba hawataki
kuutambua Uongozi wa PPFT na kutambua kwamba mimi ndiye mwenyekiti halali wa PENTECOSTE PASTORS FELLOWSHIP TANZANIA, NA
KWAMBA KUMEKUWA NA MGOGORO MKUBWA KATI YA PCT NA PPFT.
Mgogoro huu unatokana na
Katibu Mkuu wa PCT kutumwa kwa Msajili wa Vyama vya Kijamii kuzuia PPFT
Isisajiliwe, na hili sio kwetu tu, bali ninao ushahidi wa kutosha kwambwa
Uongozi wa PCT umekuwa na tabia ya kujipendekeza kwa maslahi yao kwenda katika
Ofisi ya Msajili kuishauri Serekali Isisajili Makanisa ya Kipentecoste bila
kupitia kwao.
Na Watumishi wa
Mungu wengi wameshindwa kupitia PCT kwa vile Ada inayolipishwa na PCT nikubwa kuliko ya
Serekali. Serekali ni Tsh 20,000. kwa mwaka PCT ili kuwa mwanachama lazima
ulipe 200,000. kwa mwaka.
Baba askofu Batenzi
mimi EAGT ni Mshirika na Mchungaji tu, wa Kawaida ila mimi ni Mwenyekiti wa
PPFT Kitaifa, Rejea kikao cha PCT NA PPFT Tarehe 28/3/2013 Ubungo Plaza na
kukubaliana kwamba PPFT kwa vile Sio baraza bali ni Ushirika wa Wachungaji wa
Kipentecoste hivyo PPFT itakuwa mwanachama wa PCT kwa sababu PCT ni baraza.
Natumia nafasi
hii kuwaomba Maaskofu na Wachungaji wote wa Kipentecoste kutokubaliana na
Ubinafsi, Unafiki wa Viongozi hawa wa PCT Wanaokaa vikao na kuomba kutafuta
kuonana na mimi wakati tarehe 9 na tarehe 10 Waliniita kama kiongozi wa PPFT na
kuhudhuria vikao hivyo.
Kikao cha tarehe
9 na 10 /2/2014 Niliwahoji sana kuhusu kama kweli wamepeleka Majina Ikulu
watuonyeshe wajumbe wa kikao tujue ni majina mangapi na ni akinanani
Wamependekezwa na PCT Kabla ya tarehe 11/2/2014 kujitokeza mbele ya Vyombo vya
Habari ili Kuilaumu Serekali jambo ambalo mpaka tunaenda kukutana na Vyombo
hivyo vya habari hawakutaka kuturidhisha Wajumbe wa kikao kwamba Majina
yalipelekwa.
Na hii ndio sababu mpaka leo Uongozi wa PCT
haujaweka wazi kama walipeleka Majina Ikulu ni
mangapi na ni akinanani.
KUHUSU MADAI YA
ASKOFU IKONGO KUICHONGANISHA SEREKALI NA
PCT SI KWELI.
Baba Askofu Batenzi
nakuheshimu sana, ila kwa hili ni vema wewe ukiwa Mwenyekiti wa PCT Ukasema
ukweli hata kama ukweli huo utakugharimu
ni vema kuusimamia na ndio sifa za Kiongozi Mcha Mungu na mwenye Hofu ya Mungu
ambavyo ndivyo nilivyo kuwa na kuelewa.
Nakuomba unijibu
Maswali yangu haya ndipo tutatambua Mchonganishi ni nani.
1. Mwaka
2010 wakati wa Uchaguzi mkuu wa Serekali ni
nani alieandika barua kwa jina la PCT na kuisambaza Nchi nzima kuwa
Serekali ya CCM isichaguliwe? Ni mimi au ni PCT ?
2. Barua
ya tarehe 19/3/2014 yenye maneno yanayosomeka nanukuu” HAKUNA SABABU YA
SEREKALI ILIYOKO MADARAKANI KUENDELEA KUNG'ANG'ANIA KUONGOZA NCHI” Barua hiyo Ilifikishwa Ikulu Kwa niaba ya Wapentecoste wote Tanzania
imesainiwa na Mwenyekiti wa PCT Taifa. Swali bado ni mimi naichonganisha PCT na
Serekali?
3. Barua
ambayo ni Taarifa ya PCT Taifa kwa niaba
ya Wapentecoste wote Tanzania
ya tarehe 11/2/2014 Inasema nanukuu “PCT ITATAFAKARI HATUA MADHUBUTI ZA
KUCHUKUA DHIDI YA SEREKALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI” Barua hiyo imesainiwa na
Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa PCT Taifa. Je bado mnadai Askofu Ikongo ndiye anaichonganisha
PCT na Serekali?
Mwenyekiti nadhani huo ni ushahidi wa
kutosha kwamba Uongozi wa PCT Taifa unafanya kila mbinu kuchonganisha
Wapentecoste na Serikali kwani mimi siamini kwamba Matamko hayo hapo juu ni ya
Wapentecoste wote Tanzania.
Ni wazi kwamba Uongozi wa PCT Unajaribu kuhodhi Upentecoste kanakwamba nyie
ndio mna hati miliki ya Upentecoste. Mtakuwa mnajidanganya wenyewe, kwani hata
mambo ya msingi ya kuanzishwa PCT mmeyaacha na kuanza mambo yenu wenyewe bila
hata kushirikisha Maaskofu wote na Wapentecoste Tanzania.
Nasikitika kusema
hata Wokovu wenu ninamashaka nao, kwa vile Vongozi wa PCT Mmekuwa
Waongo,Wabinafsi, na Wanafiki na kwa sababu mimi nawambia ukweli ndio sababu
mnanichukia na kuanza kukaa vikao kunijadili. Kumbukeni mliwaambia Wananchi
wote Tanzania kwamba Bonke anakuja Tanzania, nilipowaambia wambieni watu ukweli
kwamba Bonke haji, mkazusha oo Ikongo mbaya, Mlichangisha Pesa za Waumini
kwamba Bonke anakuja na ilipofika siku ya Mkutano Bonke hakuja Hamkutubu dhambi
hiyo bali mlijifunika funika ili muendelee kula pesa za Wapentecoste. Leo hii
Uongozi wa PCT hamko tayari kuweka wazi mapato na matumizi ya Pesa kiasi cha
laki mbili kila mwaka kwa makanisa 75 wanachama wa PCT bali mnamtafuta mchawi
wakati mnajiloga wenyewe.
Mwisho nimeamua kuandika
barua hii na kuweka wazi kila kitu japo mengi nimeyaacha, baada ya Wewe
Mwenyekiti kunieleza kwa njia ya simu kwamba lazima mtaniita na kunihoji katika
kikao cha tarehe 26 na 27/2/2014 kinyume chake haukuniita na kuamua kunijadili
katika kikao hicho kwa malengo ya kuficha ukweli na kunipaka matope kwa jamii
ya Wapentecoste.
Kupitia barua hii
nachukua nafasi kuwaomba Maaskofu na Wachungaji wote Tanzania
walio wanachama wa PCT kuwa makini na Uongozi wa PCT kwani Wanaichonganisha
Serekali na Wapentecoste Tanzania
kupitia Matamko wanayoyatoa bila kuwashirikisha Wanachama.
Pia ningeshauri
Kila Kanisa la Kipentecoste lililosajiliwa kihalali kuandika barua Serekalini
ya kukanusha kwamba halihusiki na Matamko makali yaliyotolewa na Viongozi wa
PCT , Na yakwamba KANISA HUSIKA
HALIKUBALIANI NA MALUMBANO NA SEREKALI. Ukihitaji barua za nakala za barua za
matamko hayo makali na ya uchonganishi kati ya Makanisa ya Kipentecoste na
Serekali nitakupatia.
Sina mengi Ila
nawatakia Viongozi wa PCT Kutubu na kurejea kwa BWANA YESU.
Nakala
Maaskofu wa Kipentecoste wote Tanzania
Wachungaji wa Kipentecoste wote Tanzania
Msajili wa Vyama vya Kijamii Tanzania
Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais
PROF. PIUS ERASTO IKONGO
MWENYEKITI PPFT TAIFA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni