Alhamisi, 22 Mei 2014

ASKOFU KAKOBE NI MCHOCHEZI



PENTECOSTE  PASTORS  FELLOWSHIP  TANZANIA
MAAZIMIO YA KIKAO CHA VIONGOZI WA DINI KILICHOKAA TAREHE 19/5/2014 KATIKA UKUMBI WA UMOJA HOSTEL MKOANI KILIMANJARO. SOMA NA UWAELIMISHE NA WENGINE WENYE KUITAKIA AMANI NCHI YETU TANZANIA,

Pamoja na kichwa cha habari hapo juu Viongozi wa DINI Mbili kubwa hapa Nchini, Wakristo na Waislamu.  Kwa pamoja baada ya  Semina iliyoendeshwa na Askofu Pius Erasto Ikongo  kutoka Dar Es Salaam, dhidi ya Matamshi na Uzushi pamoja na Ushawishi mbaya unaofanywa na Viongozi wa Dini.

Sisi Viongozi wa Dini ya Kiristo na Waislamu tuliohudhuria Semina hii Mkoani Kilimanjaro tumetoa Maazimio ya pamoja Kama ifuatavyo:-

  1. Kauli zote ambazo zimetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full  Gospel Bible Fellship Zakaria Kakobe  Dhidi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa yeye sio Mungu kuwatangazia Uma wa Tanzania ni Kosa Kubwa kwasababu ni jambo ambalo amelitunga mwenyewe na kujijibu kwa vile hakuna Mtanzania yeyete aliyewahi kusema Nyerere ni Mungu.
 Kauli hiyo ni mbaya na ina Mdhalilisha Mama yetu mpendwa Mama Maria Nyerere Ambaye Anaheshimika katika Taifa hili .

Askofu Kakobe anatakiwa Kuomba Radhi kwa Watanzania kutokana na Kauli Hiyo. Kwa pamoja Viongozi wa Dini tutaendelea kuheshimu na kuenzi Amani na Utulivu ambao tuliachiwa na Mwasisi wetu Mwalimu Nyerere. Tutaendelea Kumuombea Mama yetu Mama Maria Nyerere Mungu Ampe Afya Njema na Maisha Marefu kwa Mchango wake kwa ajili ya Taifa letu la Tanzania.

 Askofu Mkuu wa Kanisa la F G B F Kuhusu kauli yake ya kwamba ATAIDAI TANGANYIKA  IRUDI  HATA KWA KUKATWA KICHWA. Kauli hizo ni hatari na hazipaswi kutamkwa na Kiongozi au Askofu kama yeye kwani ni Kauli za KIGAIDI.
Tunamtaka Askofu Kakobe Aelewe sasa Tanzania ndio ipo kwenye Ramani ya Africa na Ulimwengu, hivyo Asiendelee kupotosha Uma wa Watanzania kwa hisia zake. Hayo ni mambo ya Wanasiasa na Asichanganye Siasa na Dini. Aidha awe na uamuzi wa kuacha Dini ili aingie kwenye Siasa. KAULI ZAKE SISI VIONGOZI WA DINI TANZANIA DINI ZOTE KUU MBILI WAKRISTO NA WAISILAMU TUMEZIKATAA.


  1. KUHUSU BUNGE LA KATIBA
Tumeona na tumezisoma Barua ambazo zimeandikwa na Maaskofu, Askofu David Batenzi wa Kanisa la Free Pentecoste Church Tanzania na Mwenyekiti wa PCT  (CPCT)  Pamoja na Askofu David Mwasota wa Kanisa la NGA  na Katibu mkuu wa PCT  (CPCT) Kuwa Mhe. Rais Amewatenga Wapentecoste, Sio za kweli ni Kauli zakupotosha  na za Uchochezi mkubwa wa kuondoa Amani na Utulivu tuliyonao katika Nchi yetu. Sisi Viongozi wa Dini zote Mbili tuliyohudhuria Semina hii hapa Mkoani Kilimanjaro, Tunawataka Askofu David Batenzi na Askofu David Mwasota Kufuta Barua hizo kwamba Siyo Wapentecoste Waliziandika Barua hizo, bali ni Mawazo yao mabaya dhidi ya Serekali yetu. Sisi Viongozi wa Dini Tunaendelea Kumheshimu Rais wetu ambaye ndio chaguo la wengi Tanzania. Tunawaomba wasitumie Mabaraza ya Wakristo kuwa Vyombo vya Kisiasa kwani Taasisi za Kidini zinatakiwa zijenge Jamii kwa Mambo ya Kiroho na Kimwili kuhusu mambo ya Mungu.

3.Viongozi wa Dini wote kwa pamoja tuliohudhuri Semina hii, Tunamtaka Askofu Batenzi na Askofu Mwasota Kufuta haraka sana kauli ya Barua walioisaini wakidai kwamba Mhe.Rais anang’ang’ania Madaraka. Rais amechaguliwa na Mamilioni ya Watanzania Kupitia Chama chake cha CCM Kwa  Kura za Kishindo Kikubwa. Kusema ana ng’ang’ania  ni Kauli Isiyokuwa na Heshima kwa Rais wetu. Pia ikumbukwe kuwa muda wa Rais Kikwete kuwa madarakani kisheria haujamalizika. Kwa hivyo siyo heshima kumtuhumu ya kuwa anang’ang’ania madaraka.


  1. Tunampongeza sana Rais wetu mpendwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa Kuliongoza Taifa hili kwa AMANI NA UTULIVU, Pia Tanzania kwa sasa Inapitika kwa Urahisi karibu Nchi nzima, hayo yote ni baadhi ya Maendeleo mengi Makubwa sana na huu ndio Ukweli usiyopingika . Mungu Akupe afya Njema ili Uliongoze Taifa hili hata tutakapofikia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

 MWISHO
Tunaomba Katiba Isiwe na Haraka Namna hii Wajumbe wote wa Tanzania Kwanza na Ukawa Wasiwe na Haraka ya Katiba. Bali Katiba Inahitaji Utulivu na Umakini na Usahihi: Katiba ndio Dira ya Taifa letu.   

ASKOFU PIUS ERASTO  IKONGO
MWENYEKITI WA PPFT TAIFA




             

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni