Alhamisi, 19 Machi 2015




  1. TAMKO WARUMI 13 : 1-
Naongea haya nikiwa Mmoja wa Wasomi  wa Binlia ngazi ta Phd hivyo siyo Professor wa heshima,Nijambo lakusikitisha sana kwa Mkristo wa kweli kuanza kushabikia Viongozi hawa wa PCT ambao walianza vizuri lakini sasa wameharibika, hawafai hata kuitwa Viongozi wa PCT au CPCT tena.

Misingi halisi ya Upentecoste hujishughulisha na mambo makubwa mawili, moja kutetea Neno la Mungu na kuhakikisha Maswala ya Kiroho yanachochewa ndani ya Wakristo.


Leo hii Viongozi hawa wa PCT walio vipofu wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia, wamefikia hatua ya kuwaunganisha Wapentekoste na Maaskofu  walevi. Ebu wewe soma Warumi 13:1-4 Amwasiye mwenye mamlaka anashindana na shauri la Mungu na lazima atapata hukumu.


Ushauri wangu Viongozi wa PCT amkeni na jitoeni ndani ya Jukwaa hilo kwani Biblia katika Ufunuo 17 Jukwaa hilo linaitwa Mnyama. PCT mnatupeleka pabaya wenzenu wana AGENDA YAO YA SIRI
TEC, CCT, na PCT au CPCT  Hawawezi kuwa na Umoja na wala hawajawahi kuwa nao, na hata wakijaribu Mungu hatawaruhusu. Wanachokifanya ni Mshikamano na si Umoja.
Askofu Bagonza amesema yeye ni Askofu wa KKKT na amedai kwamba kunae Askofu asiye julikana anatumiwa na Serikali akimaanisha Askofu Ikongo. Ni vema ikaeleweka TCF ni Jukwaa la baadhi ya Maaskofu Walevi na Wenyekuwaficha Maaskofu Waliopokea pesa  haramu za ESCROW. Soma 1. Wakoritho 2 : 15
Najisikia vizuri sana kutotambulika na Maaskofu hawa. Nilichomaanisha ni kwamba lazima Watanzania waachwe waisome katiba inayopendekezwa ndipo waamue wenyewe baada ya kuisoma. Sio kuamuliwa na kikudi cha Dini au cha Maaskofu.
Mtumishi wa Mungu kumekuwa na maswali mengi hasa juu ya Askofu Ikongo kutofautia na  jukwaa la Kikristo Tanzania . Kwa mawazo ya kawaida mtu lazima uwaze hivyo. Nilicho maanisha ni kwamba PCT Likiwa ni moja ya baraza la Kipentecoste Viongozi wake wamekuwa Viongozi vipofu wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Hakuna mtu yeyote aliye Mpentecoste wa kweli mwenye Imani ya kweli atakubaliana na PCT kujiunga na TCF. Ni jambo lililo wazi kwamba Kanisa Katoliki ni tofauti kabisa na Mifumo ya CCT na PCT.
PCT Viongozi wake wanaweza kujadiliana jambo  lolote la Kibiblia au la kimaendeleo na wakaamua kulitekeleza mara moja bila mjadala mwingine. Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki hawawezi kufanya hivyo kwani wao kila kitu kimekwisha pangwa tangu Vatkan, iwe ni Mahubiri au jambo lolote la kimaendeleo au Siasa. Hivyo haiwezekani na haitawezekana hata siku moja Mpentecoste akawa kitu kimoja na Mkatoliki. Tafadhali endelea kusomo hili somo hapo chini utafahamu madhara ya TCF kimwili na Kiroho. Pia nakuomba baada ya kusoma kwa makini ujumbe huu wote kama unaswali tafadhali usisite kuniuliza niko tayari kukujibu kwa Bishop Pius Erasto Ikongo

MTEMBEO WA EKUMENI NA UJIO WA KANISA MOJA ULIMWENGUNI NA TANZANIA IKIINGIA KATIKA MAANDALIZI YAKE KUPITIA (TCF)(THE ECUMENICAL MOVEMENT AND THE COMING ONE - WORLD CHURCH )‘‘Njoo, nitakuonyesha ADHABU YA YULE KAHABA MKUU, aketiye juu ya maji mengi. Na nikamwona MWANAMKE MMOJA AMEKETI JUU YA MNYAMA MWEKUNDU aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Mkononi mwake alikuwa ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake.


Kwenye kipaji chake cha uso palikuwa pameandikwa jina: “SIRI, BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA.’’.....Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa AMELEWA KWA DAMU YA WATAKATIFU, yaani, DAMU YA WALE WATU WALIOUAWA KWA USHUHUDA WA YESU. ……Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia. ........‘‘Yale maji uliyoyaona, yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa za watu, makutano, mataifa na lugha. Zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama, watamchukia huyo kahaba, watamfilisi na kumwacha uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kwa moto. Kwa maana Mungu ataweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia. 18 Yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkubwa unaotawala juu ya wafalme wa dunia.’’(Nabii Yohana, Ufunuo 17)Unabii wa maandiko haya unaeleza juu ya mfumo wa dini ya Uasi ambapo utakuwa na nguvu katika mataifa mengi, japo ulijihusisha na mauaji ya watakatifu wengi katika Yesu Kristo.
 

Mfumo huu unaitwa Kahaba kwa vile unajihusisha na uzinzi wa kiroho, kuwa rafiki wa dunia badala ya kuwa mkweli na mwaminifu kwa Mungu. (URAFIKI KATI YA TEC,CCT,PCT) Viongozi wa PCT wanauwezo wa kuamua,kuunda,au kubuni jambo lolote kwa faida ya Wapentecoste wote Tanzania, ila TEC hawana ruhusa tena ni mwiko kwao kufanya hivyo kwani inafahamika wazi TEC inatekeleza maagizo,mipango,Mahubiri,Siasa, kama itakavyoamriwa katika Katiba na miongozo ya Vatkani na Baba Mtakatifu. Hivyo Kanisa la Pentecoste hasa Viongozi wa PCT wanatakiwa kujitoaharaka sana kwenye jukwaa hilo wanaloliita la Wakristo wote Tanzania kwa sababu Biblia inasema wazi katika 2.Wakorintho 6 : 14 — 18. PCT Ikijiondoa TCF Itakuwa imeliokoa Kanisala Pentecoste na UKAHABA WA KIROHO, la sivyo PCT itakuwa na mahusiano ya kipagani,ufisadi wa kidunia na maovu mengi; PCT ltaharibu Kanisa la kweli na kujikusanyia mali na utajiri mwingi wa dunia, huku likijiita bado kuwa ni bi-harusi wa Kristo wakati Kristo mwenyewe amelikataa (Nabii Yohana, Ufunuo 2 : 2 : 21-22). Mfumo wa ojio wa Kanisa moja Duniani inaeleweka ya kwamba Makao makuu ya Kanisa hilo kwa mujibu wa Biblia yatakuwa katika Nchi yenye vilima saba ambayo inajulikana kuwa ni Rumi. Na kwamba mfumohuu katika sehemu za mwisho utajiunga na utawala mkuu wa Kirumi utakao anzishwa na Mnyama (mpinga Kristo).Zaidi sana mfumo huu unaitwa “SIRI,BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA kwasababu ya kutumia mfumo wa kipagani na kikahaba ulioanzishwa na Nimrodi. Christmas book page 30.

 Na leo hii duniani kuna mifumo mikuu miwili inayoitwa ya Kikristo.Mifumo Mikubwa Ya Dini Inayoitwa Ya Kikristo Katika dunia ya leo, kuna mifumo miwili mikubwa inayoitwa ya Dini Ya Kikristo. Mifumo hiyo ni Kanisa La Roman Katoliki ambalo lina jumla ya Waamini bilioni 1.3 ulimwenguni;

Baraza la Makanisa Ulimwenguni, ambalo lina jumla ya makanisa wanachama.
 a). Kanisa La Roman Katoliki Lilianzishwa katika karne ya 4 wakati Leo 1. alipotawazwa kuwa Papa wa Vatikani.Na baadaye Vatikani ikajengwa Roma na ikabakia kuwa makao makuu ya Kanisa la Roman Katoliki Ulimwenguni hadi hivi leo. Vatikani ni Nchi ndogo duniani ambayo ina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 0.44 (ekari 108.7 ) Mujibu wa takwimu za mwaka 1970, Vatikani inatawala Falme zaidi ya 690 milioni (sawa na heka 69) za watu Ulimwenguni. Mkuu wa Kanisa la Roman Katoliki na Utawala wa Vatikani ni Papa Francis. Kimsingi, Papa ana majina mengi; ikiwemo ya:-1) Suprime Pontif of the Universal Church2) Holy Fathers3) Primate of Italy4) ArchBishop And Metropolitani of the Romans province.5) Pontifix MaximusKiongozi huyu amekuwa akivaa kofia iliyoandikwa VICARVIS FILEII DEI ikiwa na maana ya badala ya mwana wa Mungu.b). Baraza La Makanisa Ulimwenguni (The world Council of Churches, WCC).Baraza la Makanisa Ulimwenguni lilianzishwa Amsterdam huko Uholanzi mwaka 1948 chini ya mkomunisti Dr. Eugene Carson Blake; baada ya juhudi za siku nyingi za kusaka umoja na makanisa ambayo si ya Kikatoliki. WCC inatumia neno la kigiriki “eukoumene” lenye maana ya ulimwengu unaozuia, au kataza.

Mtu ambaye anakuwa katika ulimwengu huu, hawezi kuwa na uamuzi wa kueleza hisia zake, bali anatakiwa apokee mambo ya Imani na kuyakubali kuwa ni kweli kama ilivyoamuliwa na mamlaka ya Kanisa (dogma).Mkutano wa kwanza wa WCC ulihudhuriwa na wawakilishi wa madhehebu mbali mbali yenye wanachama wapatao 147 kutoka Nchi 44 Ulimwenguni. Na kabla ya mwaka 1960, wakati makao makuu ya WCC yakiwa Geneva, inaripotiwa kuwa na madhehebu wanachama 252 toka katika Nchi 83 duniani, zenye uwakilishi wa watu milioni mia nne (400,000,000).Changamoto ya kwanza ya umoja huu ilianza katika mkutano wa tatu wa WCC uliofanyika katika mji mkuu wa India New Delhi Novemba 1961, wakati WCC ilipo pokea uanachama wa makanisa ya Ki-orthodox ya Urusi , Romania , Bulgaria na Poland ambao wanaaminika kuwa walikuwa Wakomunisti.Katika mkutano wa Makanisa na Vyama uliofanyika mwaka 1969 chini ya katibu wake Mkuu Philip Alford Potter wa madhehebu ya Methodist toka visiwa vya West Indian vya Dominika, ulitoa tamko la kusema, nanukuu; “revolution should be actively promoted and supported by Christians”(Official report, p.143). Tafsiri yake kwa Kiswahili: Mapinduzi lazima yafanywe na kuungwa mkono na Wakristo. “Mapinduzi”yalikusudia kung’oa vurugu za kisiasa (za kikomunist) zilizoingizwa na wakomunisti ndani ya WCC. Hivyo Muugano wa PCT,CCT,TEC na kupata jina moja lijulikanalo kama Tanzania Christian Furum (TCF) na kwa Ushahidi wa Kimaadishi kutoka Mikoani kwa mfano TCF Mwanza, TCF Mbeya na Mazungumzo katika kikao cha tarehe 8/3/2013 yaliyoambatana na Tamko la tarehe 19 Machi 2013 kwenda kwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,  Matamko mengine mengi ikiwa ni pamoja na tamko la tarehe 10 / 2/ 2015 kuwataka Wakristo kuipigia kura ya hapana  katiba inayopendekezwa , ni  wazi kwangu mimi kama Mtumishi wa Mungu Pius Erasto Ikongo na uzoefu ambao Mungu amenipa, tayari nimegundua kunamapinduzi ya Kisiasa yanayonyemelea Nchi yetu ya Tanzania kupitia Viongozi wa Kidini.Upagani aliouona Askofu Pius Ikongo Ndani Ya TCF na WCCKwa wale wanaodhani kuwa WCC au TCF ni chombo kizuri cha kuwaunganisha Wakristo bado hawaujui ukweli. WCC au TCF ni chombo cha uasi na upagani zaidi kama Ilivyojitambulisha. Baadhi ya mambo yanayodhibitisha ukweli huu ni, mkutano wa Nne wa WCC uliofanyika Upsala mwaka 1968:- 1) Mkutano huu ulimchagua Mkomunisti anayejulikana kuwa Raisi wa Baraza La Makanisa.2) WCC imejihusisha na kutoa, kugharamia, makundi ukombozi ya guelila na kigaidi yaliyo kuwepo Afrika ya Kusini na Amerika Ya kusini. Miongoni mwa makundi hayo, 19 yalikuwa Afrika na 14 ya kigaidi yalikuwa Amerika ya Kusini.3) Mwaka 1971, WCC ilimchagua mtu mwenye Imani ya Ki-Budha kuwa Katibu wa WCC huko Vietanam, Laos na Cambodia kushughulikia misaada ya Kanisa.Leo hii, kuna muongezeko wa mashirikiano kati ya WCC, Makanisa ya Roma ………. na makanisa yasiyo Roma ……. Na katika miaka ya hivi karibuni, tutashuhudia muunganiko wa makanisa yasiyo ya Ki…… kuungana na Kanisa Ka……… na kuungwa mkono na papa ili yatimie maanidko, “SIRI, BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA (Mtume Yohana, Ufunuo 17).Nje ya mifumo miwili mikuu inayojiita ya Kikristo na WCC, kuna mfumo mwingine ni wa Kanisa la Yesu Kristo, ………….. wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo (Mtume Yohana,Ufunuo 21:27). [Mfumo wa Kilokole]. EKUMENITafsiri Ya EkumeniNeno Ekumeni, limetoholewa kutoka katika lugha ya kigiriki “Oikoumene”, kueleza ulimwengu unaozuia, au kataza “Inhabited World”. Mtu ambaye amekatazwa katika ulimwengu wa Ekumeni, ni Yule ambaye hawezi na hana maamuzi ya kueleza hisia zake. Awali neno hili lilitumika kumaanisha utawala wa Kirumi, lakini baadaye likaanza kutumika kumaanisha ulimwengu wote. Katika Kamusi ya Kiswahili ya TUKI, ekumeni inatajwa kuwa ni hali ya kupenda muungano wa madhehebu yote ya Kikristo; Imani au tamko la kuleta umoja wa wakristo wote. Na katika kamusi ya AMERCAN HERITAGE, Ekumeni inatajwa kuwa ni, nanukuu; A movement promoting worldwide unity among religions through greater cooperation and improved understanding. Mtembeo unaohimiza umoja wa miongoni mwa dini Ulimwenguni kwa njia ya mashirikiano na maelewano thabiti. Hata hivyo, Katika nadharia za kitheolojia, Ekumeni ni nadharia inayotumiwa na Viongozi waandamizi wa dini ya Kikristo kwa lengo la kutaka kuleta umoja wa Imani miongoni mwa makanisa au madhehebu ya Kikristo ulimwenguni. Mabaraza Ya Ekumeni UlimwenguniMabaraza ya Ekumeni ni mkutano wa maaskofu wa makanisa au madhehebu ya kidini ambao unafanyika kwa pamoja ili kujadili fundisho la Kanisa na jinsi ya kutatua athari zinazokabili utekelezaji wa mafundisho hayo katika Jamii. Awali, mabaraza ya Ekumeni yalianzishwa kwa lengo la kuamua kuweka kipimo cha Imani na sheria ambazo baada ya kukubaliwa na Baraza la Ekumeni, zitumike kuweka nidhamu katika Kanisa kwa kuzingatia maamuzi yaliyofanywa na Baraza. Kimsingi, mafunzo yaliyokuwa yanatolewa katika mabaraza ya Ekumeni ndiyo yaliainisha mkusanyiko wa kauli na hatua za adhabu kwa kila ambaye atafanya kinyume na maamuzi ya Baraza.

Jambo ambalo kwa hapa Tanzania kama TCF ingekuwa imesajiliwa kisheria na kunauongozi kamili kama vile Mwenyekiti au katibu, lazima wangekaa na kutafuta ni adhabu gani waitoe kwa Askofu Pius Erasto Ikongo kwa kwenda kinyume na maamuzi ya mkutano wa tarehe 8/3/2013 katika ukumbi wa TEC kurasini Jijini Dar Es Salaam. Hata hivyo TCF haiwezi kuweka mwenyekiti au kuunda uongozi na kuwa na katiba kwasababu Katiba naUongozi uliopo Vatikan ndio TOSHA. Jambo hili kwa upande wa Makanisa ya Eastern Orthodox waliona ni mfumo wa Imani ambao umewekwa na Kanisa ili ukubaliwe na waamini kuwa ni kweli bila maswali.

Na kwamba, mfumo huu unaweza kutumika katika Kanisa wakati wote, na usingefaa kutumika kwa wakati wote. Mabaraza ya Ekumeni yalianzishwa na Kanisa la Roma Katoliki kwa lengo la kutaka kukabiliana na changamoto za mgawanyiko na mtengano wa madhehebu iliyoanza kujitokeza katika Kanisa la Roma Katoliki. Tangu kutokea kwamgawanyiko kati ya Kanisa la Roma Katoliki na Kanisa la Eastern Orthodox hapo mwaka 1054 B.K., kumekuwa na mtazamo tofauti wa jinsi ya kukubaliana na mapokeo ya mafundisho yanayotokana na mabaraza ya Ekumeni. Kwanza , makanisa ya Eastern Orthodox hayajawahi kukubaliana na mabaraza yeyote yanayofanywa na Kanisa Katoliki baada ya kugawanyika; hali Kanisa la Roma Katoliki likiendelea na Mabaraza yake waliamua kuendeleza mabaraza ya Ekumeni na kuwa na Komunyo kamili chini ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni na kuyatambua Kuwa ya Ekumeni hadi sasa.

Na pili, Makanisa ya Ki-Anglikana na wale wanaoukiri U-protestanti, nayo hayakubaliani na maamuzi ya baadhi ya mabaraza miongoni mwa yale 21 yaliyokwisha kufanyika.Kwa jinsi hiyo, kumekuwa na nguvu za namna mbili kuu ambazo zinazokinzana na mabaraza ya Ekumeni; moja ni ufuasi wa Madhehebu au vikundi (sectarianism) na kutaka Kugawanya au kufanya mtenganisho (separation); nyingine ni ile inayoleta ushawishi wa ulimwengu na umoja(catholicity and unity). Hali hizi mbili, zilianza kujitokeza tangu kabla ya Kipindi cha matengenezo ya Kanisa.Hali ya Madhehebu au vikundi (sectarianism) inasababishwa na mtu wa madhehebu ambaye ana mtazamo au mawazo finyu (Mlokole wa madhehebu Fulani) katika kufuata madhehebu (au kikundi). Na akisha kufaulu anataka yeye pekee aushawishi ulimwengu wote uje nyuma yake.Kwakuwa hali ya madhehebu au vikundi na mtenganisho wa hali ya kidunia na umoja zimechangia kuondoa umoja aliosema Yesu; mtandao wa ekumeni unaleta wazo la umoja katika kupambana na kuondokana na hali hizi. Hata hivyo, mambo mengine yanayoleta mgawanyo na mtengano zaidi yamechochewa na:-1) Magomvi ya Kitheolojia: Magomvi haya yanarejea msingi wa Imani ya Kanisa la kwanza la Kristo la Mitume ( Apostolic Church ). 2) Migogoro ndani ya mtembeo wa Kanisa yanayotoka na kesi za kiitikadi na (doctrinal dispute) na sera za ki-sera (policy difference), i.e. jinsi ya kuendesha Liturjia.3) Matatizo ya Itikadi na Maadili.4) Migogoro ya Kijamii na Kiutamaduni. Mtazamo Wa Kanisa La Roma Katoliki Juu Ya Changamoto Za EkumeniKatika kukabiliana na jambo hili, Kanisa la Roma Catholic kupitia Baraza lake la Ekumeni la pili ambalo lilifanyika mjini Vatikani mwaka 1962
-5 chini ya Papa Yohane wa 23; makusudi yake makuu yakiwa ni kuhuisha na kufanya matengenezo ya Kanisa Katoliki, ili kwamba mgawanyiko wa Kanisa uliotokea katika Historia usuluhishwe na kuunganishwa kwa upya, wote wawe na umoja (Yohana 17:21-23). Katika ufunguzi wa mkutano wa mtaguso wa Vatikani wa pili, Papa Yohana aliomba kusema, “Ee roho Mtakatifu fufua maajabu yako katika siku za leo, kama Pentekoste mpya” (Abott, document of Vatican II,1965).

Jambo lingine la msingi ni kuwa, Liturjia ya Kanisa iliandikwa upya na mfumo wa utawala (Serikali) ya Kanisa ulibadilishwa upya katika kuufanyia matenegenzo ule uliokataliwa na wa-protestanti, ili iwe rahisi kuwaunganisha Wa-protestanti na Wakatoliki. Kimsingi, mkutano wa mtaguso wa pili uliazimia mambo matatu ambayo yatawaunganisha na makanisa mengine yasiyo ya Kikatoliki:-1) Kuwa na ibada za nyumba kwa nyumba na Bible Study kwa lengo la kuwasaidia waamini kiroho. Mikusanyiko hii ya ibada haipaswi kuwa katika ngazi ya kisomi,na itakuwa chini ya usimamizi wa Kiaskofu.2) Kudumisha mashirikiano kati ya Wakatoliki na Waprotestanti katika shughuli za Kijamii kama vile elimu, afya, maadili na matukio ya Kiutamaduni.3) Mabadilishano ya mawazo ya kitheolijia kati ya Maaskofu na Viongozi wawakilishi wa madhehebu ya dini kama msingi wa kujenga mahusiano ili kuungana upya.Mafanikio Ya Mtaguso Wa PiliSuala la kuweka mijadala na mabadilishano ya mawazo ya kitheolijia kati ya Maaskofu na Viongozi wawakilishi wa madhehebu ya dini kama msingi wa kujenga mahusiano ili kuungana upya, lilizaa matunda baada ya miaka kumi. Mwaka 1974, ilishuhudiwa kufanyika mijadala mingi Nchini Marekani kati ya Kanisa la Roma Katoliki na uwakilishi wa madhehebu, ili kupata mawazo ya kitheolojia. Miongoni mwa madhehebu yaliyoshiriki mijadala hiyo kwa mujibu wa kitabu cha “Cellebration Annivesary of the Second Vatican Council’s Degree on Ecumenism, November 21th, 1974, Wessel) ni:-1) Southern Baptist2) American Baptist3) Lutheran4) Methodist5) Epicopalins6) Presbyterians7) Reformed8) Disciple of Christ9) Eastern OrthodoxHali ya Sasa Ya Ekumeni Ulimwenguni na Tanzania Kuna mkazo mkubwa wa makanisa kutaka kuunganisha wakristo wa madhehebu yote ya Kikristo kuwa pamoja.

Ujumbe unaotumika kusema haya ni kuwa, sisi hatuna tofuti............tunaweza kufanya kazi pamoja.Tuache tofauti zetu za theolojia pembeni, tunaweza kusaidiana katika kila jambo ambalo tunamua kulifanya kwa pamoja. Juhudi hizo zote zinafanywa chini ya mwamvuli wa Ekumeni, ukitasiriwa kuwa ni "waliojipanga kujaribu katika kuleta mashirikiano na umoja wa waamini wote katika Kristo" Ukiangalia kwa undani msingi wa juhudi za kuleta waamini kwa pamoja, ni ule WCC ambao ulihimizwa kwa nguvu katika miaka ya 1960; ambapo ulipoanza, Waprotestanti wa Kilibelali miongoni mwa madhehebu makubwa ya Kiprotestanti waliukataa baada ya kuona unakiuka mafundisho muhimu kama vile maandiko hayana makosa na uhalisia wa mandiko, kufufuliwa kwa mwili kwa Yesu Kristo hakutiliwi mkazo. Na kwa muda mrefu, Wa-Evangelical walijiondoa katika mfumo wa Ekumeni kwasababu ya kuhusisha makundi ambayo theolojia zao siyo sahihi, lakini roho ya kufanya mjadala imewaingia wa-evangelical na wamejikuta wamo ndani ya mfumo huu. Makanisa Wanachama Wa Baraza La Makanisa Ulimwenguni Walipo TanzaniaMabaraza Ya Kidini Tanganyika . Kwa upande wa madhehebu ya Kikristo, kuna mabaraza matatu ya madhehebu ya Kidini ambayo yanatambuliwa na Serikali toka miongoni mwa dini za Kikristo. Mabaraza yanayotambulika kisheria ni:-1. Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki “TanzaniaEpicospical Council” (TEC). 2. Jumuiya Ya Kikristo Tanzania“Christian Council Of Tanzania ”(CCT).3. Jumuiya Ya Wapetentekoste Tanzania “Pentecostal Council of Tanzania ”(PCT). Katika siku za hivi karibuni, Viongozi wa Mabaraza ya TEC, CCT Na PCT, wameunda Jukwaa lao ambalo linaitwa Jukwaa la Wakristo Tanzania ,“Tanzania Christian Forum” (TCF).Makanisa na Mashirika ya Kiprotestanti nchini Tanzania , ambayo yamejiunga na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (yakiwa chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania),hadi sasa yamefikia thelathini (30). Kabla ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania kuanzishwa mwaka 1964, wamisheni walikuwa na baraza lao la kimisheni la Tanganyika Missionary Council, ambalo lilianzishwa mwaka 1934. Makanisa Wanachama Wa Baraza La Makanisa UlimwenguniHadi sasa, kuna jumla ya makanisa matano (5), ambayo ni wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, “World Council Of Churches”5. Miongoni mwa makanisa haya, makanisa matatu (3) makao yake makuu yapo Tanzania ; na mengine mawili (2) hayapo Tanzania . Makanisa ambayo makao yake yapo Tanzaniani:-1. Kanisa la Anglikana Tanzania (Anglican Church of Tanzania ).2. Kanisa La Kiinjili na Kilutheri Tanzania (Evangelical Lutheran Church In Tanzania ).3. Kanisa la Moraviani (” Moravian Church in Tanzania ”)Makanisa ambayo Makao yake Hayapo Tanzania lakini yapo Tanzania ni:-1. Kanisa la Kigiriki la Kiothodox na Afrika Nzima (Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa)2. Dini ya Jamii ya Kirafiki (Religious Society of Friends/ Friends United Meeting).Makanisa ambayo ni wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni yaliyopo Tanzania ni:-1. Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT)2. Anglican Church Tanzania (ACT)3. Moravian Church in Tanzania (MCT)4. Africa Inland Church Tanzania (AICT)5. Mennonite Church in Tanzania (MCT)6. Baptist Conventional Church in Tanzania7. Salvation Army8. Church of God9. Presbyterian Church of East Africa10. Kanisa la Biblia11. Mbalizi Evangelistic Church12. Methodist Church13. Christian Brethren Assembly14. African Brotherhood Church15. Tanzania Yearly MeetingNje Ya makanisa haya kumi na tano (15), kuna mashirika ya kidini yanayojihusisha na shughuli za Kanisa kwa Kiingereza “Church Related Organizations“. Kimsingi, mashirika haya siyo makanisa, lakini kwa sehemu kubwa yanafanya huduma za kikanisa kwa kushirikiana na makanisa. Mashirika ambayo ni wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni Yaliyopo Tanzania ni:-1. Bible Society of Tanzania (BST)2. Scripture Union (SU)3. Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS)4. Young Men’s Christian Association (YMCA)5. Young Women’s Christian Association (YWCA)6. African Evangelistic Enterprise (AEE)7. Life Ministry of Tanzania8. Mission Aviation Fellowship (MAF)9. Emmanuel International10. Habitat for Humanity11. Summer Institute of Linguistic (SIL)12. Dodoma Christian Medical Centre (DCMC)13. Mennonite Central Committee (MCC)14. United Church of Canada (UCC)15. Compassion International Tanzania.

Ndugu mpendwa baada ya kusoma kwa makini utakuwa umefahamu ni kwanini Askofu Pius Erasto Ikongo hakubaliani na Matamko ya TCF, na kuendelea kuwaelimisha Wapentecoste wote Tanzania kukataa kwa nguvu kubwa kujiunga na chombo hicho wanachodai ni Jukwaa la Wakristo Tanzania . Na kama wewe kweli ni Mpentecoste wa kweli utakubaliana na mimi na tuungane kwa pamoja kuwaeleza viongozi wa PCT watutoe huko kwani wanapotupeleka ni pabaya, swali ni kwanini hawa Viongozi wa PCT wasichukue maoni kwa Wachungaji wote wa Kipentecoste ndipo wachukue uamuzi wa kujiunga na TCF ? Inavyoonyesha hawa Viongozi wanataka kuchezea Roho zetu au Imani yetu. Kama hawatatangaza kuiondoa PCT au CPCT ndani ya TCF, Nitaomba uchaguzi mkuu wa Viongozi wakuu wa PCT yani Askofu Batenzi na Askofu Mwasota. hawa waliopo tusiwarudishe kwenye Uongozi tena. Bishop Pius Erasto Ikongo Email: pierako@yahoo.com

Imechapwa na Askofu Pius Erasto Ikongo