1. TAMKO WARUMI 13 : 1-
Naongea haya nikiwa Mmoja wa Wasomi wa Binlia ngazi ta Phd hivyo siyo Professor wa heshima,Nijambo
lakusikitisha sana kwa Mkristo wa kweli kuanza kushabikia Viongozi hawa wa PCT
ambao walianza vizuri lakini sasa wameharibika, hawafai hata kuitwa Viongozi wa
PCT au CPCT tena.
Misingi halisi ya Upentecoste hujishughulisha na mambo makubwa mawili, moja kutetea Neno la Mungu na kuhakikisha Maswala ya Kiroho yanachochewa ndani ya Wakristo.
Leo hii Viongozi hawa wa PCT walio vipofu wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia, wamefikia hatua ya kuwaunganisha Wapentekoste na Maaskofu walevi. Ebu wewe soma Warumi 13:1-4 Amwasiye mwenye mamlaka anashindana na shauri la Mungu na lazima atapata hukumu.
Ushauri wangu Viongozi wa PCT amkeni na jitoeni ndani ya Jukwaa hilo kwani Biblia katika Ufunuo 17 Jukwaa hilo linaitwa Mnyama. PCT mnatupeleka pabaya wenzenu wana AGENDA YAO YA SIRI
Misingi halisi ya Upentecoste hujishughulisha na mambo makubwa mawili, moja kutetea Neno la Mungu na kuhakikisha Maswala ya Kiroho yanachochewa ndani ya Wakristo.
Leo hii Viongozi hawa wa PCT walio vipofu wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia, wamefikia hatua ya kuwaunganisha Wapentekoste na Maaskofu walevi. Ebu wewe soma Warumi 13:1-4 Amwasiye mwenye mamlaka anashindana na shauri la Mungu na lazima atapata hukumu.
Ushauri wangu Viongozi wa PCT amkeni na jitoeni ndani ya Jukwaa hilo kwani Biblia katika Ufunuo 17 Jukwaa hilo linaitwa Mnyama. PCT mnatupeleka pabaya wenzenu wana AGENDA YAO YA SIRI
TEC, CCT, na PCT au CPCT
Hawawezi kuwa na Umoja na wala hawajawahi kuwa nao, na hata wakijaribu
Mungu hatawaruhusu. Wanachokifanya ni Mshikamano na si Umoja.
Askofu
Bagonza amesema yeye ni Askofu wa KKKT na amedai kwamba kunae Askofu asiye
julikana anatumiwa na Serikali akimaanisha Askofu Ikongo. Ni vema ikaeleweka
TCF ni Jukwaa la baadhi ya Maaskofu Walevi na Wenyekuwaficha Maaskofu Waliopokea
pesa haramu za ESCROW. Soma 1. Wakoritho
2 : 15
Najisikia
vizuri sana kutotambulika na Maaskofu hawa. Nilichomaanisha ni kwamba lazima
Watanzania waachwe waisome katiba inayopendekezwa ndipo waamue wenyewe baada ya
kuisoma. Sio kuamuliwa na kikudi cha Dini au cha Maaskofu.
Mtumishi
wa Mungu kumekuwa na maswali mengi hasa juu ya Askofu Ikongo kutofautia na jukwaa la Kikristo Tanzania . Kwa mawazo ya
kawaida mtu lazima uwaze hivyo. Nilicho maanisha ni kwamba PCT Likiwa ni moja
ya baraza la Kipentecoste Viongozi wake wamekuwa Viongozi vipofu wenye kuchuja
mbu na kumeza ngamia. Hakuna mtu yeyote aliye Mpentecoste wa kweli mwenye Imani
ya kweli atakubaliana na PCT kujiunga na TCF. Ni jambo lililo wazi kwamba
Kanisa Katoliki ni tofauti kabisa na Mifumo ya CCT na PCT.
PCT
Viongozi wake wanaweza kujadiliana jambo lolote la Kibiblia au la kimaendeleo na
wakaamua kulitekeleza mara moja bila mjadala mwingine. Baraza la Maaskofu wa
Kikatoliki hawawezi kufanya hivyo kwani wao kila kitu kimekwisha pangwa tangu
Vatkan, iwe ni Mahubiri au jambo lolote la kimaendeleo au Siasa. Hivyo
haiwezekani na haitawezekana hata siku moja Mpentecoste akawa kitu kimoja na
Mkatoliki. Tafadhali endelea kusomo hili somo hapo chini utafahamu madhara ya
TCF kimwili na Kiroho. Pia nakuomba baada ya kusoma kwa makini ujumbe huu wote
kama unaswali tafadhali usisite kuniuliza niko tayari kukujibu kwa Bishop Pius
Erasto Ikongo
Email:
pierako@yahoo.com
MTEMBEO
WA EKUMENI NA UJIO WA KANISA MOJA ULIMWENGUNI NA TANZANIA IKIINGIA KATIKA
MAANDALIZI YAKE KUPITIA (TCF)(THE ECUMENICAL MOVEMENT AND THE COMING ONE -
WORLD CHURCH )‘‘Njoo, nitakuonyesha ADHABU YA YULE KAHABA MKUU, aketiye juu ya
maji mengi. Na nikamwona MWANAMKE MMOJA AMEKETI JUU YA MNYAMA MWEKUNDU aliyejaa
majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na
pembe kumi. Mkononi mwake alikuwa ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo
ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake.
Kwenye kipaji chake cha uso palikuwa pameandikwa jina: “SIRI, BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA.’’.....Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa AMELEWA KWA DAMU YA WATAKATIFU, yaani, DAMU YA WALE WATU WALIOUAWA KWA USHUHUDA WA YESU. ……Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia. ........‘‘Yale maji uliyoyaona, yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa za watu, makutano, mataifa na lugha. Zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama, watamchukia huyo kahaba, watamfilisi na kumwacha uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kwa moto. Kwa maana Mungu ataweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia. 18 Yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkubwa unaotawala juu ya wafalme wa dunia.’’(Nabii Yohana, Ufunuo 17)Unabii wa maandiko haya unaeleza juu ya mfumo wa dini ya Uasi ambapo utakuwa na nguvu katika mataifa mengi, japo ulijihusisha na mauaji ya watakatifu wengi katika Yesu Kristo.
Mfumo huu unaitwa Kahaba kwa vile unajihusisha na uzinzi wa kiroho, kuwa rafiki wa dunia badala ya kuwa mkweli na mwaminifu kwa Mungu. (URAFIKI KATI YA TEC,CCT,PCT) Viongozi wa PCT wanauwezo wa kuamua,kuunda,au kubuni jambo lolote kwa faida ya Wapentecoste wote Tanzania, ila TEC hawana ruhusa tena ni mwiko kwao kufanya hivyo kwani inafahamika wazi TEC inatekeleza maagizo,mipango,Mahubiri,Siasa, kama itakavyoamriwa katika Katiba na miongozo ya Vatkani na Baba Mtakatifu. Hivyo Kanisa la Pentecoste hasa Viongozi wa PCT wanatakiwa kujitoaharaka sana kwenye jukwaa hilo wanaloliita la Wakristo wote Tanzania kwa sababu Biblia inasema wazi katika 2.Wakorintho 6 : 14 — 18. PCT Ikijiondoa TCF Itakuwa imeliokoa Kanisala Pentecoste na UKAHABA WA KIROHO, la sivyo PCT itakuwa na mahusiano ya kipagani,ufisadi wa kidunia na maovu mengi; PCT ltaharibu Kanisa la kweli na kujikusanyia mali na utajiri mwingi wa dunia, huku likijiita bado kuwa ni bi-harusi wa Kristo wakati Kristo mwenyewe amelikataa (Nabii Yohana, Ufunuo 2 : 2 : 21-22). Mfumo wa ojio wa Kanisa moja Duniani inaeleweka ya kwamba Makao makuu ya Kanisa hilo kwa mujibu wa Biblia yatakuwa katika Nchi yenye vilima saba ambayo inajulikana kuwa ni Rumi. Na kwamba mfumohuu katika sehemu za mwisho utajiunga na utawala mkuu wa Kirumi utakao anzishwa na Mnyama (mpinga Kristo).Zaidi sana mfumo huu unaitwa “SIRI,BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA kwasababu ya kutumia mfumo wa kipagani na kikahaba ulioanzishwa na Nimrodi. Christmas book page 30.
Kwenye kipaji chake cha uso palikuwa pameandikwa jina: “SIRI, BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA.’’.....Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa AMELEWA KWA DAMU YA WATAKATIFU, yaani, DAMU YA WALE WATU WALIOUAWA KWA USHUHUDA WA YESU. ……Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia. ........‘‘Yale maji uliyoyaona, yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa za watu, makutano, mataifa na lugha. Zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama, watamchukia huyo kahaba, watamfilisi na kumwacha uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kwa moto. Kwa maana Mungu ataweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia. 18 Yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkubwa unaotawala juu ya wafalme wa dunia.’’(Nabii Yohana, Ufunuo 17)Unabii wa maandiko haya unaeleza juu ya mfumo wa dini ya Uasi ambapo utakuwa na nguvu katika mataifa mengi, japo ulijihusisha na mauaji ya watakatifu wengi katika Yesu Kristo.
Mfumo huu unaitwa Kahaba kwa vile unajihusisha na uzinzi wa kiroho, kuwa rafiki wa dunia badala ya kuwa mkweli na mwaminifu kwa Mungu. (URAFIKI KATI YA TEC,CCT,PCT) Viongozi wa PCT wanauwezo wa kuamua,kuunda,au kubuni jambo lolote kwa faida ya Wapentecoste wote Tanzania, ila TEC hawana ruhusa tena ni mwiko kwao kufanya hivyo kwani inafahamika wazi TEC inatekeleza maagizo,mipango,Mahubiri,Siasa, kama itakavyoamriwa katika Katiba na miongozo ya Vatkani na Baba Mtakatifu. Hivyo Kanisa la Pentecoste hasa Viongozi wa PCT wanatakiwa kujitoaharaka sana kwenye jukwaa hilo wanaloliita la Wakristo wote Tanzania kwa sababu Biblia inasema wazi katika 2.Wakorintho 6 : 14 — 18. PCT Ikijiondoa TCF Itakuwa imeliokoa Kanisala Pentecoste na UKAHABA WA KIROHO, la sivyo PCT itakuwa na mahusiano ya kipagani,ufisadi wa kidunia na maovu mengi; PCT ltaharibu Kanisa la kweli na kujikusanyia mali na utajiri mwingi wa dunia, huku likijiita bado kuwa ni bi-harusi wa Kristo wakati Kristo mwenyewe amelikataa (Nabii Yohana, Ufunuo 2 : 2 : 21-22). Mfumo wa ojio wa Kanisa moja Duniani inaeleweka ya kwamba Makao makuu ya Kanisa hilo kwa mujibu wa Biblia yatakuwa katika Nchi yenye vilima saba ambayo inajulikana kuwa ni Rumi. Na kwamba mfumohuu katika sehemu za mwisho utajiunga na utawala mkuu wa Kirumi utakao anzishwa na Mnyama (mpinga Kristo).Zaidi sana mfumo huu unaitwa “SIRI,BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA kwasababu ya kutumia mfumo wa kipagani na kikahaba ulioanzishwa na Nimrodi. Christmas book page 30.
Na leo hii duniani kuna mifumo mikuu miwili
inayoitwa ya Kikristo.Mifumo Mikubwa Ya Dini Inayoitwa Ya Kikristo Katika dunia
ya leo, kuna mifumo miwili mikubwa inayoitwa ya Dini Ya Kikristo. Mifumo hiyo
ni Kanisa La Roman Katoliki ambalo lina jumla ya Waamini bilioni 1.3
ulimwenguni;
Baraza la Makanisa Ulimwenguni,
ambalo lina jumla ya makanisa wanachama.
a). Kanisa La Roman Katoliki Lilianzishwa
katika karne ya 4 wakati Leo 1. alipotawazwa kuwa Papa wa Vatikani.Na baadaye
Vatikani ikajengwa Roma na ikabakia kuwa makao makuu ya Kanisa la Roman
Katoliki Ulimwenguni hadi hivi leo. Vatikani ni Nchi ndogo duniani ambayo ina
ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 0.44 (ekari 108.7 ) Mujibu wa takwimu za
mwaka 1970, Vatikani inatawala Falme zaidi ya 690 milioni (sawa na heka 69) za
watu Ulimwenguni. Mkuu wa Kanisa la Roman Katoliki na Utawala wa Vatikani ni
Papa Francis. Kimsingi, Papa ana majina mengi; ikiwemo ya:-1) Suprime Pontif of
the Universal Church2) Holy Fathers3) Primate of Italy4) ArchBishop And
Metropolitani of the Romans province.5) Pontifix MaximusKiongozi huyu amekuwa
akivaa kofia iliyoandikwa VICARVIS FILEII DEI ikiwa na maana ya badala ya mwana
wa Mungu.b). Baraza La Makanisa Ulimwenguni (The world Council of Churches,
WCC).Baraza la Makanisa Ulimwenguni lilianzishwa Amsterdam huko Uholanzi mwaka
1948 chini ya mkomunisti Dr. Eugene Carson Blake; baada ya juhudi za siku
nyingi za kusaka umoja na makanisa ambayo si ya Kikatoliki. WCC inatumia neno
la kigiriki “eukoumene” lenye maana ya ulimwengu unaozuia, au kataza.
Mtu
ambaye anakuwa katika ulimwengu huu, hawezi kuwa na uamuzi wa kueleza hisia
zake, bali anatakiwa apokee mambo ya Imani na kuyakubali kuwa ni kweli kama ilivyoamuliwa
na mamlaka ya Kanisa (dogma).Mkutano wa kwanza wa WCC ulihudhuriwa na
wawakilishi wa madhehebu mbali mbali yenye wanachama wapatao 147 kutoka Nchi 44
Ulimwenguni. Na kabla ya mwaka 1960, wakati makao makuu ya WCC yakiwa Geneva,
inaripotiwa kuwa na madhehebu wanachama 252 toka katika Nchi 83 duniani, zenye
uwakilishi wa watu milioni mia nne (400,000,000).Changamoto ya kwanza ya umoja
huu ilianza katika mkutano wa tatu wa WCC uliofanyika katika mji mkuu wa India
New Delhi Novemba 1961, wakati WCC ilipo pokea uanachama wa makanisa ya
Ki-orthodox ya Urusi , Romania , Bulgaria na Poland ambao wanaaminika kuwa
walikuwa Wakomunisti.Katika mkutano wa Makanisa na Vyama uliofanyika mwaka 1969
chini ya katibu wake Mkuu Philip Alford Potter wa madhehebu ya Methodist toka
visiwa vya West Indian vya Dominika, ulitoa tamko la kusema, nanukuu;
“revolution should be actively promoted and supported by Christians”(Official
report, p.143). Tafsiri yake kwa Kiswahili: Mapinduzi lazima yafanywe na
kuungwa mkono na Wakristo. “Mapinduzi”yalikusudia kung’oa vurugu za kisiasa (za
kikomunist) zilizoingizwa na wakomunisti ndani ya WCC. Hivyo Muugano wa
PCT,CCT,TEC na kupata jina moja lijulikanalo kama Tanzania Christian Furum
(TCF) na kwa Ushahidi wa Kimaadishi kutoka Mikoani kwa mfano TCF Mwanza, TCF
Mbeya na Mazungumzo katika kikao cha tarehe 8/3/2013 yaliyoambatana na Tamko la
tarehe 19 Machi 2013 kwenda kwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania, Matamko mengine mengi ikiwa ni
pamoja na tamko la tarehe 10 / 2/ 2015 kuwataka Wakristo kuipigia kura ya
hapana katiba inayopendekezwa , ni wazi kwangu mimi kama Mtumishi wa Mungu Pius
Erasto Ikongo na uzoefu ambao Mungu amenipa, tayari nimegundua kunamapinduzi ya
Kisiasa yanayonyemelea Nchi yetu ya Tanzania kupitia Viongozi wa Kidini.Upagani
aliouona Askofu Pius Ikongo Ndani Ya TCF na WCCKwa wale wanaodhani kuwa WCC au
TCF ni chombo kizuri cha kuwaunganisha Wakristo bado hawaujui ukweli. WCC au
TCF ni chombo cha uasi na upagani zaidi kama Ilivyojitambulisha. Baadhi ya
mambo yanayodhibitisha ukweli huu ni, mkutano wa Nne wa WCC uliofanyika Upsala
mwaka 1968:- 1) Mkutano huu ulimchagua Mkomunisti anayejulikana kuwa Raisi wa
Baraza La Makanisa.2) WCC imejihusisha na kutoa, kugharamia, makundi ukombozi
ya guelila na kigaidi yaliyo kuwepo Afrika ya Kusini na Amerika Ya kusini.
Miongoni mwa makundi hayo, 19 yalikuwa Afrika na 14 ya kigaidi yalikuwa Amerika
ya Kusini.3) Mwaka 1971, WCC ilimchagua mtu mwenye Imani ya Ki-Budha kuwa
Katibu wa WCC huko Vietanam, Laos na Cambodia kushughulikia misaada ya
Kanisa.Leo hii, kuna muongezeko wa mashirikiano kati ya WCC, Makanisa ya Roma
………. na makanisa yasiyo Roma ……. Na katika miaka ya hivi karibuni, tutashuhudia
muunganiko wa makanisa yasiyo ya Ki…… kuungana na Kanisa Ka……… na kuungwa mkono
na papa ili yatimie maanidko, “SIRI, BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO
YA DUNIA (Mtume Yohana, Ufunuo 17).Nje ya mifumo miwili mikuu inayojiita ya
Kikristo na WCC, kuna mfumo mwingine ni wa Kanisa la Yesu Kristo, ………….. wale
ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo (Mtume
Yohana,Ufunuo 21:27). [Mfumo wa Kilokole]. EKUMENITafsiri Ya EkumeniNeno
Ekumeni, limetoholewa kutoka katika lugha ya kigiriki “Oikoumene”, kueleza
ulimwengu unaozuia, au kataza “Inhabited World”. Mtu ambaye amekatazwa katika
ulimwengu wa Ekumeni, ni Yule ambaye hawezi na hana maamuzi ya kueleza hisia
zake. Awali neno hili lilitumika kumaanisha utawala wa Kirumi, lakini baadaye
likaanza kutumika kumaanisha ulimwengu wote. Katika Kamusi ya Kiswahili ya
TUKI, ekumeni inatajwa kuwa ni hali ya kupenda muungano wa madhehebu yote ya
Kikristo; Imani au tamko la kuleta umoja wa wakristo wote. Na katika kamusi ya
AMERCAN HERITAGE, Ekumeni inatajwa kuwa ni, nanukuu; A movement promoting
worldwide unity among religions through greater cooperation and improved
understanding. Mtembeo unaohimiza umoja wa miongoni mwa dini Ulimwenguni kwa
njia ya mashirikiano na maelewano thabiti. Hata hivyo, Katika nadharia za
kitheolojia, Ekumeni ni nadharia inayotumiwa na Viongozi waandamizi wa dini ya
Kikristo kwa lengo la kutaka kuleta umoja wa Imani miongoni mwa makanisa au
madhehebu ya Kikristo ulimwenguni. Mabaraza Ya Ekumeni UlimwenguniMabaraza ya
Ekumeni ni mkutano wa maaskofu wa makanisa au madhehebu ya kidini ambao
unafanyika kwa pamoja ili kujadili fundisho la Kanisa na jinsi ya kutatua
athari zinazokabili utekelezaji wa mafundisho hayo katika Jamii. Awali,
mabaraza ya Ekumeni yalianzishwa kwa lengo la kuamua kuweka kipimo cha Imani na
sheria ambazo baada ya kukubaliwa na Baraza la Ekumeni, zitumike kuweka nidhamu
katika Kanisa kwa kuzingatia maamuzi yaliyofanywa na Baraza. Kimsingi, mafunzo
yaliyokuwa yanatolewa katika mabaraza ya Ekumeni ndiyo yaliainisha mkusanyiko
wa kauli na hatua za adhabu kwa kila ambaye atafanya kinyume na maamuzi ya
Baraza.
Jambo
ambalo kwa hapa Tanzania kama TCF ingekuwa imesajiliwa kisheria na kunauongozi
kamili kama vile Mwenyekiti au katibu, lazima wangekaa na kutafuta ni adhabu
gani waitoe kwa Askofu Pius Erasto Ikongo kwa kwenda kinyume na maamuzi ya
mkutano wa tarehe 8/3/2013 katika ukumbi wa TEC kurasini Jijini Dar Es Salaam.
Hata hivyo TCF haiwezi kuweka mwenyekiti au kuunda uongozi na kuwa na katiba
kwasababu Katiba naUongozi uliopo Vatikan ndio TOSHA. Jambo hili kwa upande wa
Makanisa ya Eastern Orthodox waliona ni mfumo wa Imani ambao umewekwa na Kanisa
ili ukubaliwe na waamini kuwa ni kweli bila maswali.
Na
kwamba, mfumo huu unaweza kutumika katika Kanisa wakati wote, na usingefaa
kutumika kwa wakati wote. Mabaraza ya Ekumeni yalianzishwa na Kanisa la Roma
Katoliki kwa lengo la kutaka kukabiliana na changamoto za mgawanyiko na
mtengano wa madhehebu iliyoanza kujitokeza katika Kanisa la Roma Katoliki.
Tangu kutokea kwamgawanyiko kati ya Kanisa la Roma Katoliki na Kanisa la
Eastern Orthodox hapo mwaka 1054 B.K., kumekuwa na mtazamo tofauti wa jinsi ya
kukubaliana na mapokeo ya mafundisho yanayotokana na mabaraza ya Ekumeni. Kwanza
, makanisa ya Eastern Orthodox hayajawahi kukubaliana na mabaraza yeyote
yanayofanywa na Kanisa Katoliki baada ya kugawanyika; hali Kanisa la Roma
Katoliki likiendelea na Mabaraza yake waliamua kuendeleza mabaraza ya Ekumeni
na kuwa na Komunyo kamili chini ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni
na kuyatambua Kuwa ya Ekumeni hadi sasa.
Na
pili, Makanisa ya Ki-Anglikana na wale wanaoukiri U-protestanti, nayo
hayakubaliani na maamuzi ya baadhi ya mabaraza miongoni mwa yale 21
yaliyokwisha kufanyika.Kwa jinsi hiyo, kumekuwa na nguvu za namna mbili kuu
ambazo zinazokinzana na mabaraza ya Ekumeni; moja ni ufuasi wa Madhehebu au
vikundi (sectarianism) na kutaka Kugawanya au kufanya mtenganisho (separation);
nyingine ni ile inayoleta ushawishi wa ulimwengu na umoja(catholicity and
unity). Hali hizi mbili, zilianza kujitokeza tangu kabla ya Kipindi cha
matengenezo ya Kanisa.Hali ya Madhehebu au vikundi (sectarianism) inasababishwa
na mtu wa madhehebu ambaye ana mtazamo au mawazo finyu (Mlokole wa madhehebu
Fulani) katika kufuata madhehebu (au kikundi). Na akisha kufaulu anataka yeye
pekee aushawishi ulimwengu wote uje nyuma yake.Kwakuwa hali ya madhehebu au
vikundi na mtenganisho wa hali ya kidunia na umoja zimechangia kuondoa umoja
aliosema Yesu; mtandao wa ekumeni unaleta wazo la umoja katika kupambana na
kuondokana na hali hizi. Hata hivyo, mambo mengine yanayoleta mgawanyo na
mtengano zaidi yamechochewa na:-1) Magomvi ya Kitheolojia: Magomvi haya
yanarejea msingi wa Imani ya Kanisa la kwanza la Kristo la Mitume ( Apostolic
Church ). 2) Migogoro ndani ya mtembeo wa Kanisa yanayotoka na kesi za
kiitikadi na (doctrinal dispute) na sera za ki-sera (policy difference), i.e.
jinsi ya kuendesha Liturjia.3) Matatizo ya Itikadi na Maadili.4) Migogoro ya
Kijamii na Kiutamaduni. Mtazamo Wa Kanisa La Roma Katoliki Juu Ya Changamoto Za
EkumeniKatika kukabiliana na jambo hili, Kanisa la Roma Catholic kupitia Baraza
lake la Ekumeni la pili ambalo lilifanyika mjini Vatikani mwaka 1962
-5
chini ya Papa Yohane wa 23; makusudi yake makuu yakiwa ni kuhuisha na kufanya
matengenezo ya Kanisa Katoliki, ili kwamba mgawanyiko wa Kanisa uliotokea
katika Historia usuluhishwe na kuunganishwa kwa upya, wote wawe na umoja
(Yohana 17:21-23). Katika ufunguzi wa mkutano wa mtaguso wa Vatikani wa pili,
Papa Yohana aliomba kusema, “Ee roho Mtakatifu fufua maajabu yako katika siku
za leo, kama Pentekoste mpya” (Abott, document of Vatican II,1965).
Jambo
lingine la msingi ni kuwa, Liturjia ya Kanisa iliandikwa upya na mfumo wa
utawala (Serikali) ya Kanisa ulibadilishwa upya katika kuufanyia matenegenzo
ule uliokataliwa na wa-protestanti, ili iwe rahisi kuwaunganisha Wa-protestanti
na Wakatoliki. Kimsingi, mkutano wa mtaguso wa pili uliazimia mambo matatu
ambayo yatawaunganisha na makanisa mengine yasiyo ya Kikatoliki:-1) Kuwa na
ibada za nyumba kwa nyumba na Bible Study kwa lengo la kuwasaidia waamini
kiroho. Mikusanyiko hii ya ibada haipaswi kuwa katika ngazi ya kisomi,na
itakuwa chini ya usimamizi wa Kiaskofu.2) Kudumisha mashirikiano kati ya Wakatoliki
na Waprotestanti katika shughuli za Kijamii kama vile elimu, afya, maadili na
matukio ya Kiutamaduni.3) Mabadilishano ya mawazo ya kitheolijia kati ya
Maaskofu na Viongozi wawakilishi wa madhehebu ya dini kama msingi wa kujenga
mahusiano ili kuungana upya.Mafanikio Ya Mtaguso Wa PiliSuala la kuweka
mijadala na mabadilishano ya mawazo ya kitheolijia kati ya Maaskofu na Viongozi
wawakilishi wa madhehebu ya dini kama msingi wa kujenga mahusiano ili kuungana
upya, lilizaa matunda baada ya miaka kumi. Mwaka 1974, ilishuhudiwa kufanyika
mijadala mingi Nchini Marekani kati ya Kanisa la Roma Katoliki na uwakilishi wa
madhehebu, ili kupata mawazo ya kitheolojia. Miongoni mwa madhehebu
yaliyoshiriki mijadala hiyo kwa mujibu wa kitabu cha “Cellebration Annivesary
of the Second Vatican Council’s Degree on Ecumenism, November 21th, 1974,
Wessel) ni:-1) Southern Baptist2) American Baptist3) Lutheran4) Methodist5)
Epicopalins6) Presbyterians7) Reformed8) Disciple of Christ9) Eastern
OrthodoxHali ya Sasa Ya Ekumeni Ulimwenguni na Tanzania Kuna mkazo mkubwa wa
makanisa kutaka kuunganisha wakristo wa madhehebu yote ya Kikristo kuwa pamoja.
Ujumbe
unaotumika kusema haya ni kuwa, sisi hatuna tofuti............tunaweza kufanya
kazi pamoja.Tuache tofauti zetu za theolojia pembeni, tunaweza kusaidiana
katika kila jambo ambalo tunamua kulifanya kwa pamoja. Juhudi hizo zote
zinafanywa chini ya mwamvuli wa Ekumeni, ukitasiriwa kuwa ni "waliojipanga
kujaribu katika kuleta mashirikiano na umoja wa waamini wote katika Kristo"
Ukiangalia kwa undani msingi wa juhudi za kuleta waamini kwa pamoja, ni ule WCC
ambao ulihimizwa kwa nguvu katika miaka ya 1960; ambapo ulipoanza,
Waprotestanti wa Kilibelali miongoni mwa madhehebu makubwa ya Kiprotestanti
waliukataa baada ya kuona unakiuka mafundisho muhimu kama vile maandiko hayana
makosa na uhalisia wa mandiko, kufufuliwa kwa mwili kwa Yesu Kristo hakutiliwi
mkazo. Na kwa muda mrefu, Wa-Evangelical walijiondoa katika mfumo wa Ekumeni
kwasababu ya kuhusisha makundi ambayo theolojia zao siyo sahihi, lakini roho ya
kufanya mjadala imewaingia wa-evangelical na wamejikuta wamo ndani ya mfumo
huu. Makanisa Wanachama Wa Baraza La Makanisa Ulimwenguni Walipo
TanzaniaMabaraza Ya Kidini Tanganyika . Kwa upande wa madhehebu ya Kikristo,
kuna mabaraza matatu ya madhehebu ya Kidini ambayo yanatambuliwa na Serikali
toka miongoni mwa dini za Kikristo. Mabaraza yanayotambulika kisheria ni:-1.
Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki “TanzaniaEpicospical Council” (TEC). 2.
Jumuiya Ya Kikristo Tanzania“Christian Council Of Tanzania ”(CCT).3. Jumuiya Ya
Wapetentekoste Tanzania “Pentecostal Council of Tanzania ”(PCT). Katika siku za
hivi karibuni, Viongozi wa Mabaraza ya TEC, CCT Na PCT, wameunda Jukwaa lao
ambalo linaitwa Jukwaa la Wakristo Tanzania ,“Tanzania Christian Forum”
(TCF).Makanisa na Mashirika ya Kiprotestanti nchini Tanzania , ambayo
yamejiunga na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (yakiwa chini ya Jumuiya ya
Kikristo Tanzania),hadi sasa yamefikia thelathini (30). Kabla ya Jumuiya ya
Kikristo Tanzania kuanzishwa mwaka 1964, wamisheni walikuwa na baraza lao la
kimisheni la Tanganyika Missionary Council, ambalo lilianzishwa mwaka 1934.
Makanisa Wanachama Wa Baraza La Makanisa UlimwenguniHadi sasa, kuna jumla ya
makanisa matano (5), ambayo ni wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni,
“World Council Of Churches”5. Miongoni mwa makanisa haya, makanisa matatu (3)
makao yake makuu yapo Tanzania ; na mengine mawili (2) hayapo Tanzania .
Makanisa ambayo makao yake yapo Tanzaniani:-1. Kanisa la Anglikana Tanzania
(Anglican Church of Tanzania ).2. Kanisa La Kiinjili na Kilutheri Tanzania
(Evangelical Lutheran Church In Tanzania ).3. Kanisa la Moraviani (” Moravian
Church in Tanzania ”)Makanisa ambayo Makao yake Hayapo Tanzania lakini yapo
Tanzania ni:-1. Kanisa la Kigiriki la Kiothodox na Afrika Nzima (Greek Orthodox
Patriarchate of Alexandria and All Africa)2. Dini ya Jamii ya Kirafiki
(Religious Society of Friends/ Friends United Meeting).Makanisa ambayo ni
wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni yaliyopo Tanzania ni:-1.
Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT)2. Anglican Church Tanzania
(ACT)3. Moravian Church in Tanzania (MCT)4. Africa Inland Church Tanzania
(AICT)5. Mennonite Church in Tanzania (MCT)6. Baptist Conventional Church in
Tanzania7. Salvation Army8. Church of God9. Presbyterian Church of East
Africa10. Kanisa la Biblia11. Mbalizi Evangelistic Church12. Methodist
Church13. Christian Brethren Assembly14. African Brotherhood Church15. Tanzania
Yearly MeetingNje Ya makanisa haya kumi na tano (15), kuna mashirika ya kidini
yanayojihusisha na shughuli za Kanisa kwa Kiingereza “Church Related
Organizations“. Kimsingi, mashirika haya siyo makanisa, lakini kwa sehemu kubwa
yanafanya huduma za kikanisa kwa kushirikiana na makanisa. Mashirika ambayo ni
wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni Yaliyopo Tanzania ni:-1. Bible
Society of Tanzania (BST)2. Scripture Union (SU)3. Tanganyika Christian Refugee
Service (TCRS)4. Young Men’s Christian Association (YMCA)5. Young Women’s
Christian Association (YWCA)6. African Evangelistic Enterprise (AEE)7. Life
Ministry of Tanzania8. Mission Aviation Fellowship (MAF)9. Emmanuel
International10. Habitat for Humanity11. Summer Institute of Linguistic
(SIL)12. Dodoma Christian Medical Centre (DCMC)13. Mennonite Central Committee
(MCC)14. United Church of Canada (UCC)15. Compassion International Tanzania.
Ndugu
mpendwa baada ya kusoma kwa makini utakuwa umefahamu ni kwanini Askofu Pius
Erasto Ikongo hakubaliani na Matamko ya TCF, na kuendelea kuwaelimisha
Wapentecoste wote Tanzania kukataa kwa nguvu kubwa kujiunga na chombo hicho
wanachodai ni Jukwaa la Wakristo Tanzania . Na kama wewe kweli ni Mpentecoste
wa kweli utakubaliana na mimi na tuungane kwa pamoja kuwaeleza viongozi wa PCT
watutoe huko kwani wanapotupeleka ni pabaya, swali ni kwanini hawa Viongozi wa
PCT wasichukue maoni kwa Wachungaji wote wa Kipentecoste ndipo wachukue uamuzi
wa kujiunga na TCF ? Inavyoonyesha hawa Viongozi wanataka kuchezea Roho zetu au
Imani yetu. Kama hawatatangaza kuiondoa PCT au CPCT ndani ya TCF, Nitaomba
uchaguzi mkuu wa Viongozi wakuu wa PCT yani Askofu Batenzi na Askofu Mwasota. hawa
waliopo tusiwarudishe kwenye Uongozi tena. Bishop Pius Erasto Ikongo Email: pierako@yahoo.com
Imechapwa
na Askofu Pius Erasto Ikongo
Email:
pierako@yahoo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni